Ruka hadi kwenye maudhui makuu

CD YA JAY-Z AKICHAPWA NA WIFI YAZUA BALAA

Mitandao ya kijamii imewaka moto kufuatia kanda ya video iliyozuka ikionyesha dadake mwanamuziki wa kimataifa Beyonce Knowles , Solange Knowles akimchapa makonde mwanamuziki Jay-Z ambaye pia ni shemeji yake katika lifti.

Hoteli ambako kisa hicho kinadaiwa kutokea mjini New York, 'The Standard Hotel' ilisema kuwa inachunguza ambavyo kanda ya kisa kilichotokea ndani ya Lifti iliweza kusambazwa baada ya kanda hiyo ya video kuzuka katika mtandao mmoja wa udaku TMZ.


Hata hivyo kanda hiyo haikuwa na sauti bali ilionyesha tu kitendo cha dadake Beyonce akimpacha Jay-Z na hata kujaribu kumpiga teke mara mbili wakiwa ndani ya lifti hiyo pamoja na Beyonce na mlinzi mmoja wa Jay-Z aliyejaribu kumzuia Solange.

Kanda hiyo ilizuka baada ya Beyonce aliyekuwa ameambatana na mumewe Jay Z pamoja na Solange kuhudhuria tamasha la kifahari mjini New York tarehe tano Mei.
Dadake Beyonce Solange Knowles
Mlinzi wa Jay-Z anaonekana katika kanda hiyo akijaribu kumzuia Solange mwenye umri wa miaka 27 aliyeonekana kuwa na hasira mno kutomchapa Jay-Z amwenye umri wa miaka 44 akiwa amesimama kando ya mkewe wa miaka sita Beyonce.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, taarifa kutoka kwa maafisa wa hoteli ambamo kisanga hicho kilitokea walielezea kukasirishwa na mtu ambaye aliisambaza kanda hiyo kwenye internet na hata kutishia kumchukulia hatua pindi atakapojulikana.

"tumeshtushwa sana na kukasirishwa na mtu aliyekiuka sheria zetu za faragha ambazo wageni wetu wanathamini sana, '' ilisema taarifa kutoka kwa wakuu wa hoteli hiyo.

"tunachunguza hali hiyo na pia yeyote atakayepatikana na hatia ataadhibiwa vikali.''
Wasimamizi wa Beyonce walikataa kuzingumzia kisa hicho.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC