Okwi aipongeza Yanga kumsajili Okello


Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Anorld Okwi, amefunguka na kuipongeza klabu ya Yanga kuinasa saini ya kiungo wa ushambuliaji, Allan Okello huku akidai kuwa wamefanya kazi kubwa na wamepata mchezaji bora.

Kwani sio kitu rahisi kumshawishi rais wa klabu ya Vipers, Lawrence Mulindwa ambaye alikuwa akiamini watamuuza Okello barani Ulaya au nchi za Afrika ya Kaskazini kutokana na uwezo alionao.

"Kwenye ukweli lazima useme kuwa va uongozi wa Yanga unastahili pongezi kwa usajii wa nyota Allan Okelo wa Uganda.

Huku ni kukomaa kwa viongozi wa Yanga, kingine ni kitendo cha Rais wa Yanga, Eng. Hersi Saidi kuingilia kati mwenyewe kimemfanya Mulindwa kuwa mpole''.
Alisema Okwi, ambaye pia amewahi kukipiga Yanga SC.