Clara Luvanga apiga hat trick nyingine Al Nassr
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania Clara Luvanga hii leo ameifungia Hat Trick Klabu yake ya Al Nassr Women na kuisaidia kushinda 7-1 dhidi ya Eastern Flames kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake nchini Saudi Arabia .
.
Clara Luvanga amefikisha mabao 15 kwenye Ligi hiyo akiwa ndiye kinara wa mabao huku Klabu yake ikishika nafasi ya kwanza kwenye Msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza michezo minane.
