Simba yanunua basi jipya la kisasa, lina choo ndani
Kupitia ukurasa rasmi wa Simba SC Tanzania wameweka picha ya Basi jipya la klabu hiyo likiwa halina nembo yoyote ya mdhamini wa Klabu.
Kwa mbele likiwa na maandishi ya "SIMBA SC" ,na katika plate number ikiandikwa "16 APRIL 2025".
Kumbuka mdhamini mkuu ambaye ni kampuni ya kubashiri ya M-BET hatokuwa na Simba SC kuelekea msimu ujao hivyo huenda Kuna dili kubwa Mnyama anasaini na Moja ya kampuni kubwa zaidi.
