Moussa Camara atimkia Guinea na majeruhi yake
Golikipa namba moja wa mnyama Simba SC, Moussa Pinpin ameondoka alfajiri ya leo kulekea nchini Ivory Coast kwaajili ya kujiunga na kambi ya timu ya taifa ya Guinea kuelekea mechi za kufuzu Kombe la Dunia
Simba iliwaomba Guinea kumuacha Camara Dar es salaam ili apate muda wa matibabu zaidi lakini Guinea wamesema watamfanyia Vipimo na kumtibia ili kuona kama wataweza kumtumia.
