Kimanzi apewa mkono wa kwaheri Tabora United
Klabu ya Soka ya Tabora United,inayoshiriki ligi kuu ya NBCPL imetangaza kuachana na aliyekuwa Kocha wao mkuu, Francis Kimanzi pamoja na aliyekuwa msaidizi wake Yusuph Chipo.
Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo, uamuzi huo umechukuliwa kutokana na mwenendo usioridhisha wa klabu hiyo tangu kuanza kwa msimu huu wa 2024/24.
Francis kimanzi aliisaidia Mathare United kurejea katika ligi kuu ya FKFPL na baadaye kuhamia Tabora United katika msimu wa 2024-2025

