Huyu ndio Nassor Saadun Hamoud wa Azam FC
Huyu Nassor Saadun ni mzaliwa wa Temeke Dar es Salaam,tarehe 23 Machi 2001, pengine simulizi yake ilianzia pale kwa timu ya vijana ya Mtibwa Sugar ile ya 2017/18,
Miongoni mwa timu tishio kuwahi kutokea kwa soka la vijana ikiwa na nyota kama Onesmo Mayaya, Aboutricker, Dickson Job na Wengineo.
Akiwa na timu ya vijana ya Mtibwa alikuwa anacheza winga lakini mara kadhaa alikuwa akicheza mshambuliaji wa kati akipishana na Abdul Haule na Onesmo mayaya,
Waliokuwa wanashuhudia mazoezi ya vijana wa Mtibwa pale kwenye uwanja wa Volcano basi wanajua kwamba Saadun alikuwa hakubali kufanyiwa mabadiliko mpaka afunge goli 3.
Lakini pia Saadun alipita kwenye klabu ya Tersana inayoshiriki Ligi daraja la pili huko Misri na hii ilikuwa msimu wa 2018/19 na baadae kutimkia huko Serbia kunako Belgrade Zone huku akitumikia vilabu kama Žarkovo,Šumadija Aranđelovac, na baadae kupelekwa kwa mkopo Vyškov na kisha baadae kurudi nchini.
Kwa sifa zake kocha yoyote yule anaweza kumtumia maeneo tofauti tofauti na kumpa performance nzuri.
Miongoni mwa sifa zake ni kasi,uwezo wa kumiliki mpira,nguvu, huku kikubwa zaidi ni jicho sahihi la kuupeleka mpira anapotaka uendee,mpaka sasa kwenye ligi ya kandanda ya NBC amefunga magoli mawili lakini tunzenii hii atafunga zaidi ya goli 10 kama atapata game time.
