MANZOKI AITOSA SIMBA NA KUTUA UAE
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati mwenye asili ya DR Congo, Cesar Lobi Manzoki (27) Amekamilisha Usajili wake wa kujiunga na Klabu ya Hatta Sports Club inayoshiriki Ligi kuu ya UAE kwa Mkataba wa Mwaka Mmoja na Nusu Kwa Uhamisho huru akitokea Klabu ya Dallian Professional FC ya China.
Manzoki ambaye amewahi kuvitumikia vilabu vya AS Maniema union, AS Vita Club za DR Congo, pamoja Vipers SC ya Uganda Anajiunga na klabu ya Hatta Club iliyoi nafasi ya pili kutoka mwisho ya (13) wakiwa na alama (5) kwenye Mechi (12) kwenye ligi yenye timu (14) inayoongozwa na Klabu ya Al Wasl walio kileleni na points zao (30) Katika Mechi (12).
