MZAMIRU KUONGEZA MIWILI
Kiungo wa Simba, Mzamiru Yassin ataongeza kandarasi ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa miaka miwili zaidi mwishoni mwa mwezi huu.
Mzamiru Yassin anamaliza mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi mwishoni mwa msimu huu na atakuwa Mchezaji huru (Free agent) ambapo Singida Fountain Gate inajiandaa kutuma ofa kwenye Menejiment ya Mchezaji huyo.
Uongozi wa Simba umepitia ripoti ya Mwalimu umeridhishwa na kiwango cha Mzamiru Yassin na ataongezewa mkataba mpya, Simba itaendelea kuwaongezea mikataba wachezaji ambao wanaamini bado ni msaada kwa klabu hiyo.
