MARUMO GALLANTS WAPIGWA KWAO 2-0
Wapinzani wa Yanga SC katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya nusu fainali timu ya Marumo Gallants wamefungwa mabao 2-0 na Mamelodi Sundowns katika uwanja wake wa nyumbani.
Mchezo huo wa Ligi Kuu Afrika Kusini, Mamelodi wamepata magoli yao kupitia kwa Thadeo Morena na Themba Zwane na kuwatia mkosi wa kufungwa kwenye uwanja wake wa nyumbani.
Marumo na Mamelodi ni wawakilishi pekee wa Afrika Kusini katika michuano ya kimataifa. Marumo itakutana na Yanga Mei 10 katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam na zitarudiana Mei 17 nchini Afrika Kusini.
Mamelodi ambao wanashiriki Ligi ya mabingwa Afrika, wataumana na Wydad Casablanca ya Morocco.
