BATAMBUZE MCHEZAJI BORA VPL SEPTEMBA 2017

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Beki wa pembeni wa Singida United, Mganda, Shafik Batambuze ametangazwa kuwa mchezaji bora wa VPL kwa mwezi Septemba mwaka huu baada ya kuwashinda Ibrahim Ajibu wa Yanga na Mohamed Issa wa Mtibwa Sugar alioingia nao fainali.

Batambuze aliyejiunga na Singida United msimu huu, ameshinda tuzo hiyo hasa kutokana na kuiwezesha timu yake kukamata nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

Juhudi binafsi za mchezaji huyo zimemfanya kushinda tuzo hiyo, kwa maana hiyo sasa Batambuze atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni mbili ambazo hutolewa kwa mchezaji bora wa kila mwezi, mwezi Agosti tuzo hiyo ilienda kwa kiungo mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi

Shafik Batambuze (Kulia) 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons