Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MKUU wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Yanga SC Jerry Cornely Murro amelikingia kifua Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF ambalo leo limemwandikia barua afike shaurini Jumamosi ijayo. TFF imemwandikia barua msemaji huyo wa Yanga kwamba ahudhurie ofisi za Shirikisho hilo Uwanja wa Karume Dar es Salaam kujibu tuhuma zinazomkabili Murro anadaiwa kutoa maneno ya kejeli kwa Shirikisho hilo. Lakini barua aliyotumiwa Murro haionyeshi kama anaitwa na kamati gani ya TFF zaidi ya kusema anaitwa na kamati, Naye Murro amesema hakubaliani na barua hiyo na yupo tayari kupambana na yeyote mwenye kutaka kumchafua yeye na Yanga
Kwa habari na matangazo tunapatikana Kariakoo jijini Dar es Salaam au piga +255 652 626627 au +255 755 522 216 barua pepe princehoza@gmail.com