MLUNDWA AMCHARUKIA USTAADH
MKURUGENZI wa Shirikisho la ngumi za kulipwa nchini PST Emmanuel Mlundwa (Pichani) amemjia juu mkurugenzi wa kamisheni ya ngumi nchini Yassin Abdallah ;Ustaadh; kufuatia kauli zake za kutaka kusitisha pambano lililoandaliwa na shirika lake.
Akizungumza na mtandao huu juzi, Mlundwa amesema kuwa bondia Fransis Cheka atapamnda ulingoni tarehe 10 kama ilivyopangwa kuaizchapa na bondia kutoka Malawi na pia atacheza na Mmarekani tarehe 30 kama ilivyopangwa.
Mlundwa amesisitiza kuwa hakuna mtu yeyote atakayeweza kutibua pambano aliloliandaa yeye kufanyika, Lakini anashangaa kumsikia Ustaadh akijinadi kutolitambua pambano hilo la tarehe 10 huku akitumia vyombo vya habari kuvuruga.
Hata hivyo Mlundwa amesema pambano lipo pale pale na kama likishindwa kufanyika basi pambano la tarehe 30 kati ya Cheka na Mmarekani pia halitafanyika