Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Singida Black Stars nao wahamia Zanzibar

Machapisho ya hivi karibuni

Ndayiragije avunja mkataba Police FC

Kocha raia wa Burundi Étienne Ndayiragije amekatisha Mkataba Wake na Police FC ya Nchini Kenya Baada ya kuifundisha klabu hiyo kwa Miezi 11. Étienne Ndayiragije alijiunga na Klabu hiyo Mwishoni Mwa Mwezi Novemba ambapo aliikuta ikiwa nafasi ya mwisho katika michezo nane iliyokuwa imecheza kwenye Ligi Kuu ya Kenya. Kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo ilishinda Kombe la Ligi Kuu Kenya na kuiwakilisha nchi katika Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika. Katika Michuano ya klabu Bingwa Afrika, walitolewa na Al Hilal SC ya Sudan katika raundi ya pili. Inaelezwa kuwa Étienne Ndayiragije kuna timu ambayo iko inawinda saini yake ili aweze kuwa Kocha Mkuu ingawa bado haijawekwa wazi ni Klabu ipi. Etienne Ndayiragije

Makocha wa Simba na Yanga matawi ya juu Algeria

Klabu 4 za Algeria zimefanikiwa kuingia hatua ya Makundi ya mashindano ya CAF CAF Champions League zilizoingi ni MC Alger inayonolewa na Rulani Mokwena, JS Kabylie inayonolewa na Josef Zinnbauer. CAF Confederation Cup zilizofuzu ni CR Belouizdad inayonolewa na Sead Ramović aliyewahi kuinoa Yanga na timu ya USM Alger inayonolewa na Abdelhak Benchikha ambaye aliwahi kuinoa Simba SC.

Yanga yailaza Mtibwa Sugar

MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. Pongezi kwa wafungaji wa mabao ya leo – wachezaji wapya, beki Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ aliyesajiliwa kjutoka kwa watani, Simba SC dakika ya 38 na kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Chad, Célestin Ecua aliyesajiliwa kutoka Zoman FC ya Ivory Coast dakika ya 83. Baada ya mchezo huo, Tshabalala ambaye anafahamika pia kwa jina lingine la utani, Zimbwe Junior alikabidhiwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi kwa kiwango kizuri alichokionyesha leo. Kwa ushindi wa leo, Yanga inafikisha pointi saba katika mchezo wa tatu baada ya kuichapa Pamba Jiji mabao 3-0 kwenye mchezo wa kwanza na sare ya bila mabao na Mbeya City kwenye mchezo uliofuata Jijini Mbeya. Kwa upande wao Mtibwa Sugar waliorejea Ligi Kuu msimu huu baada ya msimu mmoja wa kucheza Championship wanabaki na pointi zao tano za mechi tano ...

Azam FC yahamia New Amaan Zanzibar

KLABU ya Azam FC imeamua kuutumia Uwanja wa New Amaan Complex kwa ajili ya mechi zake za hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika baada ya Uwanja wao wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. “Mashabiki wetu na wakazi wa Zanzibar kwa ujumla tunawaletea burudani ya mechi zetu za Kombe la Shirikisho Afrika zilizobakia kwa msimu huu 2025/26, baada ya kuuchagua Uwanja wa New Amaan Complex kama uwanja wetu wa nyumbani,” imesema taarifa ya Azam FC leo na kuongeza; “Zanzibar tunakuja kuanzia hatua ya makundi, kaeni tayari kutupokea! Hii ni zamu ya Azam.

Twiga Stars yafuzu fainali za kombe la mataifa Afrika Morocco 2026

TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars leo imefanikiwa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika Wanawake 2026 nchini Morocco baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, Ethiopia jioni ya leo Uwanja wa Taifa wa Dire Dawa mjini Dire Dawa katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Pili na ya mwisho ya mchujo. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo mshambuliaji wa Trabzonspor ya Uturuki, Diana Lucas Msewa na kwa matokeo hayo Tanzania inafuzu WAFCON ya mwakani kwa ushindi wa jumla wa 3-0 kufuatia ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam – mabao ya washambuliaji Aisha Juma Mnunka wa Simba Queens dakika ya 23 na Jamila Rajab Mnunduka wa JKT Queens dakika ya 56. Inakuwa mara ya tatu kwa Twiga Stars kufuzu Fainali za WAFCON baada ya mwaka 2010 nchini Afrika Kusini na 2024 nchini Morocco na mara zote walitolewa katika hatua ya makundi.

Pamba Jiji yapewa ushindi wa mezani Ligi Kuu bara

Klabu ya Pamba Jiji imepewa alama tatu na magoli matatu baada ya mchezo wao dhidi ya Dodoma Jiji kushindwa kuendelea ukichezwa dakika 6 tu. Mchezo huo ulindwa kuendelea kutokana na umeme kukatika dakika ya 6, hivyo kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi ya bodi ya ligi kuu (TPLB) imewapata Pamba alama tatu na magoli matatu kwa kosa la wenyeji (Dodoma Jiji) kushindwa kuuandaa mchezo vyema.