Ruka hadi kwenye maudhui makuu

NABII MUSA KIONGOZI WA WANAISRAEL

Inaandikwa na Fikiri Salum

MUSA aliishi miaka ya 1250 hivi KK akawa kiongozi wa wana Israel walipoondoka nchini Misri kukimbilia nchi ya Kanaani iliyoitwa Palestina na Israel baadaye.

Hasa Torati na vitabu vingine vya biblia vinasimulia habari zake, pia Kurani inamtaja Musa katika Aya 502, Waisrael waliishi Misri kama wageni tu zaidi ya miaka mia nne (Mdo 7-6-16 wakiongezeka kiasi cha kuwatisha wenyeji wao ambao walianza kuwafanya watumwa mwaka 1,300 hivi KK, kwa mujibu wa biblia, katika kuwakomboa utumwani, Mungu alijionesha mtetezi wa haki za masikini.

Pamoja na kushurutishwa kufanya kazi walizozipenda, ilitolewa amri ya kuua watoto wote wa kiume, ingawa mpango huo haukutekelezwa sawa sawa (KUT 1:7-22).

Mmoja kati ya watoto waliookolewa katika mpango wa kuua watoto wa kiume ni Musa wa kabila la Lawi (KUT 2:1-10; EB 11:23: Mdo 7:17-22), mama wa Musa alimficha mtoto halafu akamweka ndani ya kikapu mtoni.

Hatimaye mtoto akaokotwa na binti Farao na kulelewa kama mtoto wa Kifalme, lakini alijua asili yake, baadaye akawa Afisa wa Kimisri alipaswa kukimbilia Jangwani kwa kabila la Wamidiami akaolea huko (KUT 2:11-22: EB 11:24-27: Mdo 7:23-29). alipokuwa kwenye mlima Sinai akaitwa na Mungu kutoka ndani ya kichaka kinachowaka moto bila kuteketea.

Mungu alimchagua kurudi Misri na kuongoza watu wake katika utumwa wa Farao, Mungu akasisitiza aende mwenyewe, naye atatumia uwezo wake wa Kimungu kumlazimisha Farao.

Kadiri Musa alivyoomba, Mungu alimfunulia jina lake takatifu YHWH ambalo linaeleweka kiasi tu, kama vile fumbo la Mungu mwenyewe (KUT 2:23-20: Mdo 7;30-35.

MAPIGO YA WAMISRI

Mungu alipomtuma Musa kwa Farao alijua tayari huyo atakataa kuwaruhusu Waisrael waende zao, mpaka aone mapigo yake kwa Wamisri, kwa kuwa ulihitajika muda kuleta ukombozi iliwabidi Waisrael wawe na imani na subira hadi ahadi za Mungu zitimie.

Waisrael walianza kunung' unika (KUT 5:1-6:1) hata hivyo Mungu akaendelea na mpango wake, maajabu aliyoyatenda huwa yanatokea Misri lakini si yote kwa wakati mmoja wala si kwa kiasi kile alichosababidha Musa kwa fimbo yake (KUT 6:28-7:7).

Tuna orodha hayo lakini kwa kawaida yanahesabiwa kumi maji ya mto Naili kuwa mekundu kama damu, vyura kujaa nchi, chawa, nzi, tauni, majipu, mvua ya mawe, nzige, Giza na hatimaye kifo cha wazaliwa wa kwanza wa kiume wa watu na wanyama.

Adhabu hizo ziliwapata Wamisri, lakini si Waisrael hivyo ilikuwa wazi kuwa Mungu anagua watu wake na watu waovu, katika pigo la kumi Waisrael waliopolewa kwa kuipaka milango yao damu ya mwanakondoo (KUT 11;1+10 Mdo 7:36-37: EB 11:28).

Hivyo Mungu aliwaandaa watu kupokea imani kwa Yesu Kristo, mwanakondoo wa kweli na mkombozi wa waliokuwa watumwa wa dhambi, shetani na kifo (Yoh 19:36: /Kar 5:7;/ Pet 1:18-20) hiyo ni wazi katika ibada iliyoagizwa ifanyike kila mwaka (KUT 12:1-14) yaani Waisrael wale nyuma ya mwanakondoo dume asiye na hila, pamoja na mkate usiotiwa chachu na mboga ya majani machungu.

Yesu akaifanya ibada hiyo iwe ibada kwa Agano jipya la milele, akiagiza tuifanye kwa ukumbusho wake, si tena kwa ukumbusho wa kutoka Misri (1 Kor 11:28-26).

SAFARI YA KWENDA NCHI YA AHADI

KUT 12:24-42 inasimulia Waisrael wote walivyokimbia Misri pamoja na mifugo yao waliposikia mayowe kutoka nyumba za majirani wao wote.

INAENDELEA


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe