Inasemekana kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Elie Mpanzu raia wa DR Congo, ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili baada ya kuonesha kiwango kizuri katika mechi za karibuni.
Tajiri wa klabu hiyo Mohamed Dewji "MO Dewji" akishirikiana na mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo Crensetius Magori wamemalizana na nyota huyo ambaye alikuwa akihusishwa na Yanga.
