Goli pekee lililofungwa na mshambuliaji Laurindo Maria Aurelia Depu usiku huu limeiwezesha klabu ya Yanga SC kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons ya mkoani Mbeya katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Kwa matokeo hayo Yanga SC inaendelea kuongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 35 huku ikiwa imecheza mechi 13, ushindi kwa Yanga haukuwa rahisi kwani iliwachukua dakika ya 76 kuandika bao la ushindi.
Vijana wa Tanzania Prisons inayonolewa na beki wa zamani wa klabu hiyo na Yanga pamoja na timu ya taifa, Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa "Fuso" ilicheza vizuri kwa kulinda lango lao muda wote.
