Veron Mosengo-Omba amestaafu rasmi kama Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF.
Sura muhimu inafungwa katika katika shirikisho la soka Afrika CAF ambapo Mosengo-Omba alikuwa na jukumu muhimu katika usimamizi na mageuzi ya kandanda ya Afrika.
Kwasasa nguvu anazielekeza katika majukumu mengine ya kisoka akiwa miongoni mwa wagombea wa Rais wa shirikisho la soka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Uchaguzi ambao ungefanyika mwezi huu ulisogezwa mbele baada ya FIFA kubaini uwepo wa uhaba wa fedha za kuandaa uchaguzi huo.
