Ruka hadi kwenye maudhui makuu

ASILI YA BINADAMU

Inaandikwa na Fikiri Salum

DOMENI+ Eukaryota, Himaya- Animalis (wanyama) Fails: chordata (wanyama) au (wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni) Ngeli; Mamalia (wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao) Oda: primatei (wanyama wanaofanana kiasi na binadamu).

Familia ya Hominoidea au (wanyama kama binadamu) Fakilia: hominidea (wako na mnasaba na binadamu).

Nusufamilia: hominidea (wanaofanana sana na binadamu) Jenasi; Homo, Linnaeus, 1758 Spishi! H Sapiens, Linnaeus 1758 Numspishi: H S, Sapiens.

Binadamu (pia mwanadamu) ni neno linalomaanisha mwana wa Adamu anayeaminiwa na dini ya Uyahudi, Ukristo na Uislamu kuwa ndiye mtu wa kwanza.

BINADAMU KADIRI YA SAYANSI

Kisayansi jina hilo linaweza kutumika kwa maana ya Homo Sapiens Ili kumtofautisha na viumbe wengine wa Jenasi Homo ambao wote walitoweka walau miaka 12,000 hivi iliyopita.

Watu wote walioko leo hii ni spishi Ile Ile na tofauti zinazoonekana kati ya maumbile yao katika sehemu mbalimbali za dunia ni kidogo tu.

Utafiti juu ya DNA umethibitisha kwamba binadamu wote wametokana na watu waliokiwepo Afrika walau miaka 250,000 hivi iliyopita.

Kwa namna ya pekee, upimaji wa DNA ya mviringo, ambayo kila mmoja anarithi kwa mama tu, ulionyesha kuwa binadamu wote waliopo duniani wanachangia mama mmoja aliyewahi kuishi miaka 130,000 hivi iliyopita.

Halafu upimaji wa kromosomu Y, ambayo kila mwanamume anarithi kwa baba tu, ulionyesha kuwa wanaume wote wanachangia baba mmoja aliyewahi kuishi walau miaka 70,000 hivi iliyopita, kidogo kabla ya baadhi ya watu kuanza kuhama bara la Afrika na kuenea Asia labda kufuata pwani za bahari ya Hindi.

Hata hivyo, miaka hii ya mwisho imegundulika katika baadhi ya wanaume wenye asili ya makabila ya Wabangwa na Wambo (Cameroon), Afrika ya Kati) aina ya Kromosomu Y, tofauti sana na Ile ya wanaume wengine wote waliowahi kupimwa, kiasi kwamba kukadiria imetofautiana miaka 350,000 hivi iliyopita.

Vilevile upimaji wa DNA ya mstari kwa jumla umeonyesha uwezekano wa kwamba baadhi ya binadamu wa leo, wale wasio wa kusini mwa Sahara, wana asilimia 1-6 ya urithi wa kibiolojia kutoka kwa aina nyingine za Homo, hususani Homoneanserthlensis, Ile ya pango la Denisova na Ile iliyorithiwa na baadhi ya watu wa visiwa vya Andaman (India).

Kama hao waliweza kweli kuzaliana na Homo Sapiens maana yake walikuwa spishi moja na yeye, hapo asili ya binadamu inatakiwa kuhesabiwa ya zamani zaidi sana kuliko 200,000 iliyofikiriwa kwanza.

INAENDELEA 


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe