Meneja wa Habari wa klabu ya Yanga SC, Ali Shabani Kamwe amewaponda baadhi ya wachambuzi na mashabiki wa soka wanaodai timu yake imeshuka uwezo na kocha wao hafai endapo timu hiyo inatoka sare wakati watani zao wakitoka sare wanadai ligi ni nzuri na Ina ushindani.
"Yanga wakipata sare: timu imeshuka uwezo, kocha hamna, usajili mbovu.
Kolo wakipata sare: ligi nzuri, hamna maigizo, wamepambana sana.
Yanga wakishinda: wananunua wapinzani, marefa wabovu, wanabebwa.
Kolo wakishinda: usajili dirisha dogo umelipa, mabingwa wapya, timu imekuwa bora.
Azam akishinda au akipata sare: ibenge bonge la kocha.
Maneno ya Msemaji wa Young Africans Sports Club
Ali Kamwe
