Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Pedro Soares Gonçalves ametoa orodha ya wachezaji (7) ambao watakosekana kwenye mchezo wa hapo kesho dhidi ya Namungo FC kutokana na majeraha akiwemo Prince Dube pamoja na Pacome Zouzoua.
"Kwa bahati mbaya tuna baadhi ya wachezaji wenye majeraha ambao hawakuweza kuja na timu
Aziz Adambwile alipata majeraha kidogo, bado tunaendelea kufuatilia hali yake lakini tuna matumaini si tatizo kubwa.
Edmund John pia ana majeraha aliyopata wiki iliyopita huenda akarejea mazoezini baada ya siku chache.
Pacome Zouzoua alipata maumivu baada ya kugongana na kipa katika mchezo uliopita, hivyo hayuko katika hali nzuri kwa sasa.
Kibwana Shomari na Abutwalib Mshery pia ni wagonjwa na hakuweza kusafiri.
Prince Dube alikuwa na tatizo la kiafya wakati wa mazoezi.
Clement Mzize anaendelea vizuri huku akipata uangalizi wa umakini kabla hajarejea tena kuwa nasi"
-Pedro Gonçalves, Kocha wa klabu ya Yanga
