Nyota wa basketball Tanzania, Hasheem Thabeet amechaguliwa kuwa rais wa chama cha mpira wa kikapu Tanzania (TBF) baada ya kushinda kinyanganyiro hicho katika uchaguzi uliofanyika leo jijini Dodoma.
Katika uchaguzi huo Hasheem ameibuka mshindi baada ya kupata kura 34 kati ya 60 zilizopigwa na wajumbe wote.
Hashem kwa sasa anachezea timu ya kikapu ya Dar City ambayo inatarajiwa kucheza fainali za ‘BAL’ kwenye michezo itakayochezwa kuanzia Machi 27 nchini Afrika Kusini.
Wengine walioshinda katika uchaguzi huo Mohamed Kisui (Makamu wa Rais), Mwenze Fiston Kabinda (Katibu Mkuu) na Simon Milondo (Naibu Katibu Mkuu).

