Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Dudubaya, Wastara kimeeleweka

Penzi la Wastara(43) na Dudubaya(51) limeanza kuchukua sura mpya baada ya Wastara kutoa kauli inayodokeza tayari amepanga kufunga ndoa na Dudubaya ambaye ni mwanamuziki mkongwe wa kizazi kipya(Bongofleva). Wastara ndie alianza kuweka wazi penzi lao kisha Dudubaya kuthibitisha baadaye

Wastara ambaye baba yake alikuwa mwarabu, hata hivyo haijajulikana bado ndoa ya safari hii wamepanga iwe ya dini gani kwani yeye Wastara ni muislamu wakati Dudubaya ambaye jina lake halisi ni Godfrey Tumaini, ni mkiristo

ITAKUWA NDOA YA NNE

Wastara ambaye alizaliwa mwaka 1983, alipokuwa secondary kidato cha pili aliacha shule huko Morogoro, akiwa na miaka 16 aliolewa na mwanaume kutoka Zanzibar ambaye alimzidi sana umri ingawa ndoa haikudumu ilivunjika ndani ya muda mfupi

Baada ya kufanya kazi pamoja katika filamu kadhaa, 2008/2009 Wastara alifunga ndoa ya pili na Sajuki aliyekuwa mwigizaji wa filamu, hadi Sajuki alipoaga dunia 2013, walijaaliwa mtoto mmoja

January Mwaka 2016, Wastara aliolewa na Sadifa Juma aliyekuwa mbunge wa jimbo la Donge, Zanzibar hata hivyo ndoa yao haikudumu waliachana, hawakupata mtoto pamoja

Wastara ana watoto wengine akiwemo mmoja aliyezaa na Solo Thang mwanamuziki mkongwe wa hip-hop Tanzania ambaye kwasasa anaishi nchini Ireland kwa miaka takribani ishirini. Penzi lao lilikuwa mwanzoni mwaka miaka ya 2000s

Mbali na hayo, Wastara aliwahi pia kuwa katika mahusiano na Bond Suleiman mtangazaji na mwigizaji wa Kibongo kabla hajaolewa ghafla ndoa ya tatu hali ikiyosababisha Bond kukiri kutaka kujiu@ baada ya mrembo huyo kwenda kuolewa na mwanaume mwingine

Kwa upande wa Dudubaya alishawahi kuwa na mke kabla, pia ana watoto kutoka mahusiano yake ya awali


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa