SPIKA wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan ‘Zungu’, amesema Baba Levo limethibitishwa ni jina rasmi la Mbunge wa Kigoma Mjini, Clayton Revocatus Chipando.
-
Spika Zungu ametoa kauli hiyo bungeni leo Januari 27, 2026 alipokuwa akimuita Mbunge huyo kuulizwa swali la nyongeza bungeni, ambapo Spika alisema wamethibitisha kwamba hilo ni jina rasmi la Mbunge huyo baada ya kulifanyia kiapo.
-
Wakati akiapa kwenye Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 13 Novemba 2025, Mbunge huyo alitaja jina lake la Baba Levo kwenye kiapo chake, lakini Spika alimuelekeza aliondoe kwani sio jina rasmi.
