Wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika, Yanga SC usiku huu imeilazimisha sare ya bila kufungana 0-0, wenyeji JS Kabylie ya Algeria na kufanikiwa kuongoza kundi B.
Yanga SC ambao katika mchezo wake wa kwanza uliofanyika uwanja wa New Amaan Stadium Zanzibar dhidi ya FAR Rabat na kushinda 1-0, imecheza vizuri na kuondoka na pointi moja ugenini.
Watani zao Simba SC wataingia dimbani keshokutwa itakapocheza na Stade Malien ya Mali mchezo utakaopigwa mjini Bamako, nchini Mali.
