Mshambuliaji hatari wa Stade Malien ya Mali, Taddeus Nkeng Fomakwang (25) yuko kwenye rada za Yanga ndani ya dirisha dogo la usajili.
Taddeus Nkeng Fomakwang ni raia wa Cameroon, na amewahi kupita kwenye timu za vijana za FC Porto ya Ureno, HJK ya Finland na Carabobo ya Colombia.
Nyota huyo anaweza kucheza nafasi zote tatu za mbele.
