Andiko la digital Manager wa Klabu ya Young Africans Priva Abiud Shayo "Privaldinho" likimzungumzia mchambuzi wa masuala ya kandanda Hans Rafael wa Crown FM.
"Hans Hans Hans.
Mtu akipitia post zako za jana baada ya Yanga kushinda na baada ya makolo kushinda, Inafikirisha kidogo ndugu yangu. Juzi wakati makolo wanateseka dhidi ya JKT hukusema lolote baya dhidi yao. Hukuongelea chochote kuhusu Mpanzu kuwa katika mechi 8 amefunga bao moja pekee ikiwa ni mechi tatu kwenye ligi hajafanya kitu.
Hukusema ubutu wa Mukwala. Ulichagua angle ya kuwapambana makolo.
Hukujadili clear chances walizokosa makolo.
Kipind cha kwanza JKT walifanikiwa kuwadhibiti
Makolo. Makolo walipata shot on target moja tu na shot off target 1. Ulikaa kimya
Badala yake ulisifia kiwango cha baadhi ya nyota wake. Sio dhambi kusifia ila unasifiaje?
Baada ya mapambio yako, kilichofuata sio tena uchambuzi ispokuwa ukawa mhamasishaji wa makolo. Nanukuu maneno yako
“keep fighting, keep knocking, keep believing.....hiyo ndio maana halisi ya timu kubwa. Haijalishi umetanguliwa ila ni kupambana hadi dakika ya mwisho, hakika leo Simba wamecheza kibingwa, wameonyesha Mamba mentality”
Brother, JKT uliwapa hii hamasa pia? Imekuwaje? Mchambuzi unawezaje kutoa kauli za namna hii? Huoni kama unawakosea heshima JKT? Kwamba makolo walikuwa bora kwa JKT kwa tofauti ya goli 1?
Huo umwamba wa Makolo ni upi? How? Difference ya goli moja mdogo wangu? Hivi unajua katika mechi ambayo makolo walikuwa na wastani mdogo wa pasi ni dhidi ya JKT? Hivi unajua katika mechi ambazo Kolo amefunga magoli machache ni dhidi ya JkT? Hivi unajua mechi pekee ya ligi ambayo kolo ameruhusu bao ni dhidi ya JKT?
Takwimu zinaonesha wastani wao wa pasi dhidi ya JkT ni 68 watsani mdogo zaidi msimu huu.? Hizi sifa umetoa kwenye papatu papatu hii hii?
Hivi unajua baada ya mechi 6 JKt juzi ndio amefanikiwa kupata bao dhidi ya Kolo? Kwanini unatumia nguvu kubwa kuforce agenda ya kwamba makolo wanacheza vizuri kuliko Yanga? Unawaogopa? Una balance?. Sijamaliza..! Narudi".

