Rapa na Mfanyabiashara maarufu Sean "Diddy" Combs amekamatwa akinywa pombe akiwa ndani ya Gereza la Fort Dix, kulingana na taarifa zilizotolewa na TMZ.
Maafisa wa gereza wamesema kuwa staa huyo alitengeneza pombe yake mwenyewe kwa kuchanganya mchanganyiko wa Fanta, sukari, na tufaha ( Apple) sawa na mchanganyiko ambao wafungwa wengine huzitengeneza na kuziruhusu kukaa kwa takriban wiki mbili hadi ziwe pombe.
Awali, walipanga kumhamisha Diddy kwenda kitengo kingine cha gereza kutokana na tukio hilo, lakini uamuzi huo umegeuzwa. Kabla ya hukumu yake, Diddy aliwaambia majaji kwamba amekuwa hana tabia ya kunywa pombe kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 25.
