Kocha Milutin Sredojević ameisaini mkataba wa kuinoa timu ya ES Sétif kwa mkataba wa msimu mmoja na nusu.
Mtaalamu huyo raia wa Serbia ni mmoja wa Makocha waliopata heshima barani Afrika.
Aliwahi kuwa kocha wa Orlando Pirates, SC Villa, Zamalek, St. George, Young Africans, Al Hilal, na zaidi aliiongoza Uganda kurejea AFCON baada ya miaka 39.
Kwa upande wa timu ya taifa pia alizisimamia Zambia, Libya na Rwanda, akijenga timu imara na zenye nidhamu.
