Anaandika George Ambangile
Dimitri Pantev amejipotezea alama tatu yeye mwenyewe leo mchezo wa mwisho dhidi ya Jkt Tanzania alicheza bila mshambuliaji wa mwisho alihangaika kupata matokeo mpaka alipofanya mabadiliko ya kumuingiza Sowah, Kibu Morice timu ikaanza kufunguka.
Leo kilicho muaminisha kurudia alichokishindwa kwenye mechi ya muhimu ni nini ?
Unacheza dhidi ya timu inayoshambulia sio bahati mbaya ama hawa ni utamaduni wao kushambulia wakiwa ugenini ama kwao.
Una Sowah, Mwalimu, Mukwala unawaachaje walinzi wa Petro Atletico wawe huru kucheza, kuanzisha mashambulizi na kuisukuma timu yao icheze upande wa Simba ilihali wewe upo nyumbani?
Dakika zaidi ya 20 - 30 za kwanza timu haifanyi pressing, Maema hafiki kwenye matukio, back pass nyingi mpaka mashabiki wanakasirika kwa kelele nje zilitosha kumuamsha.
Nafasi za wazi zinatengenezwa nyingi ila hakuna wa kumalizia lakini bado Pantev aliamini mpango kazi wa kutumia viungo wengi na False Number 9
Kilichotokea ......
Hata muda wa mabadiliko tayari Petro walikuwa wameshazoea kucheza na Simba hawakuwa na presha tena, hali ya hewa imetulia kimesalia kijua cha jioni tu.
Kilichokuwa kimesalia kuiokoa Simba ni ubora tu wa wachezaji wa Simba kuamua timu ifunge ama ifungwe .
Na kweli ubora wao ukaamua Simba ifungwe.
