Kwa taarifa ambazo ninazo CEO wa Klabu ya Simba, Bi Zubeda Sakuru ameongezewa mkataba kuendelea na nafasi hiyo pasipo ya baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba Kujua.
Mkataba wa CEO wa awali ulipaswa kuisha Julai 2025, halafu Bodi ijadili upya nafasi yake.
Kwa mujibu wa taarifa ya awali ya Simba Sports Club Bi Zubeda Sakuru alipewa miezi sita ya Kukaimu nafasi hiyo ambayo iliachwa na Mrwanda Francois Regis baada ya kusitishiwa mkataba wake.
Taarifa ambazo ninazo kwenye moja ya Kikao cha Bodi wakati wanataka kujadili nafasi ya CEO baada ya miezi sita yake ya kukaimu kuisha akatokea mjumbe mmoja wa Bodi akasema haina haja ya kujadili maana mbona tayari Bi Zubeda Sakuru ameshapewa mkataba wa kuendelea na nafasi hiyo jambo ambalo liliwashangaza baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.
