Inasemekana klabu ya Yanga SC inaweza kuachana na mshambuliaji wake Andy Boyeli raia wa DR Congo baada ya kushindwa kuonesha kiwango chake.
Boyeli alisajiliwa kwa mkopo kutoka kwenye klabu ya Shenkhume United ya Afrika Kusini na tayari Yanga wameshaijulisha klabu hiyo mpango wa kumuacha.
Wanajangwani hao watasajili mshambuliaji mpya katika dirisha dogo la Januari.
