Wekundu wa Msimbazi, Simba SC usiku huu imeilalua timu ya Namungo FC mabao 3-0 mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Ikiwa chini ya kocha msaidizi Seleman Matola, Simba ilitangulia kwa bao la Chamou Karaboue dakika ya 44 kabla ya Rushine De Reuck dakika ya 61 kufunga la pili wakiwa wote ni mabeki wa kati.
Lakini mshambuliaji wa Wydad Casablanca, Seleman Mwalimu Gomez aliyepo Simba kwa mkopo, aliiandikia bao la tatu dakika ya 85, kwa matokeo hayo Simba inakaa kileleni ikiwa na pointi 6 na mechi mbili