Uongozi wa klabu ya Yanga umeampa mechi tatu kocha mkuu wa klabu hiyo Romain Folz ili kubadilisha mwenendo wa klabu hiyo na kama si hivyo watamfuta kazi mara moja.
Hata hivo kocha Folz hajaridhishwa na kitendo hiko kwani wameonekana hawana Imani naye hivo anaweza akaamua kuondoka zake ndani ya Jangwani.
Kama Romain Folz ataendelea kusalia Jangwani anatakiwa kufanya kazi ya zaida kukiandaa kikosi hiko kabla ya kurejea kwa Ligi baada ya mapumziko ya kimataifa.
Inakumbukwa kuwa hii imekuja kutokana na matokeo ya sare tasa ya 0-0 katika mchezo wao wa Ligi jioni ya Jana uliopigwa katika uwanja wa CCM Sokoine jijini Mbeya dhidi ya wenyeji wao Mbeya City kutoka huko huko jijini Mbeya.