Imefahamika kwamba kocha wa zamani wa Yanga SC, Nasreddine Nabi amekuja nchini kutalii tu na wala Hana mpango wa kujiunga na klabu ya Simba au Yanga.
Taarifa za Nabi kuhitajika na Simba zilienea jana pale tu alipoonekana jijini Dar es Salaam, lakini mtu wa karibu na kocha huyo ambaye pia ameinoa Kaizer Chief ya Afrika Kusini amedai kwamba amekuja kupumzika na wala SI kujiunga na Simba.