BAADA ya Kocha Nasreddine Nabi kuonekana nchini Tanzania kwa siku za hivi karibuni akihusishwa na klabu baadhi; hatimaye kocha mwenyewe amefafanua zaidi kuwa yupo nchini kwa masuala yake binafsi.
“Nimeona watu wanasema nimekuja hapa kwa ajili ya Simba, wengine wanasema Yanga, hapana! Nipo hapa kwa safari yangu binafsi, nadhani hii ni mara ya tatu nakuja hapa," alisema Nabi
Akaongeza; “Tanzania ni kama nyumbani ndio maana napenda sana kuja hapa, tangu nimefika sijakutana na kiongozi yeyote wa Simba wala Yanga, nikimaliza mambo yangu nitaondoka.”