Mshambuliaji Fiston Mayele kaweka kamba mbili na kuisaidia Pyramids FC kuondoka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Wenyeji APR FC Katika mchezo wa CAFCL
Pale Jukwaani Kulikuwa na mshikaji wake Jesus Moloko waliye cheza pamoja wakiwa Young Africans, Moloko alienda kumshuhudia PREDATOR FISTON MAYELE Akiifanya kazi yake naye akaifanya vyema pale Katika Dimba la Stade Régional Nyamirambo
Baada ya Mchezo kumalizika FISTON MAYELE Alitambua uwepo wa Jesus Moloko na akaenda kumpatia jezi yake.
Jesus Moloko hivi sasa anaichezea AS Kigali ya Rwanda.