Inasemekana kwamba kocha Miguel Gamondi wa Singida Black Stars anaweza kuigharimu timu hiyo na kukatwa pointi sita ilizonazo kwakuwa ana adhabu ya kufungiwa na Bodi ya Ligi wakati anainoa Yanga SC.
Mara ya mwisho,Miguel Gamondi anaondoka Tanzania alifungiwa mechi 3 na adhabu ya Tsh milioni 2,000,000.
Kwa mujibu wa CEO wa Bodi ya Ligi,adhabu ya hela walikatwa Yanga,Lakini vipi kuhusu adhabu ya Gamondi?
Amerudi na tumeona tayari mechi 2 za Ligi amekaa kama kocha mkuu wa Singida Black Stars,vipi BODI YA LIGI imesahau?
Kanuni iko kimya? Nini kimefanya Gamondi kukaa benchi mechi 2 za Ligi Kuu Tanzania Bara huku akiwa na adhabu?
Wapinzani waliofungwa na Singida Black Stars wakisimama na kuleta hili hoja,watapewa haki yao kikanuni?
Tunatamani Bodi ya Ligi itupe majibu sahihi kwenye Hili la Gamondi ili tusirudi tulipotoka.