Klabu ya Dodoma Jiji imepigwa faini ya jumla ya TZS milioni 15 baada ya kucheza michezo ya Ligi Kuu bila kuwa na kocha mwenye sifa na ujuzi unaotakiwa.
Adhabu hiyo imetokana na klabu hiyo kushiriki michezo mitatu tofauti, dhidi ya KMC, TRA United, na Coastal Union, ambapo kwa kila mchezo imepigwa faini ya TZS milioni tano.