Timu ya Azam FC usiku huu imeshindwa kuutumia vema uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo Mbweni jijini Dar es Salaam baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu bara.
Bao la Feisal Salum Abdallah maarufu Feitoto dakika ya 43 liliitanguliza kileleni lakini walishindwa kung' ang' ania bomba baada ya dakika ya 90 kijana wake wa zamani Paul Peter Kasunda kuisawazishia JKT Tanzania na kulazimisha sare na kuduwaa.