Uongozi wa Klabu ya Azam FC ya Dar es salaam umeiandikia barua bodi ya ligi ukilalamikia uamuzi mbovu kwenye mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania uliopigwa jana Octoba 1,2025.
Katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya kufungana bao moja kwa moja Azam FC imeyalalamikia matukio kadhaa ambayo hayakuamuliwa kwa usahihi.
Barua hiyo imewasilishwa kwa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi leo asubuhi.