TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa kirafiki kwenye kilele cha tamasha ka Mbeya City Day leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na beki wa kati, Muivory Coast, Landry Ahoutou Angenor Zouzou dakika ya 17 na mshambuliaji Mtunisia, Taieb Ben Zitoun dakika ya 90’+2.
Huo unakuwa mchezo wa sita wa kujipima kwa Azam FC chini ya kocha mpya, Jean-Florent Ibenge raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika maandalizi ya msimu mpya.
Mechi tano za awali Azam FC ilitoa sare ya bila mabao na Vipers FC ya Uganda, ilishinda 2-0 dhidi ya APR na penalti 4-3 dhidi ya Polisi kufuatia sare ya 1-1 na kufungwa 2-1 na AS Kigali zote kwenye ziara ya Rwanda Jijini Kigali.
Mchezo wa kwanza Azam FC ikifungwa 2-1 na JKT Tanzania katika kambi yake ya awali mjini Karatu Jijini Arusha.