MKUTANO Mkuu wa kawaida wa klabu ya Yanga utafanyika Jumapili ya Septemba 7 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Taarifa ya Yanga iliyosainiwa na Rais wa klabu hiyo, Hersi Ally Said imesema kwamba Mkutano huo ni kwa mujibu wa Ibara ya 20 ya Katiba ya klabu hiyo ya mwaka 2021.