Kiungo mshambuliaji raia wa Afrika Kusini ambaye alikua anaitumikia timu ya Mamelod Sundown maarufu kama Masandawana Neo Maema ametambulishwa kama mchezaji mpya wa timu ya Simba SC Wekundu wa Msimbazi inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania NBC siku ya leo kwenye majengo maarufu ambayo yalijengwa kipindi cha mfalme Falao yenye umbo la Piramidi.
Mchezaji huyo inaaminika kuwa atakuja kuongeza kitu katika safu ya ushambuliaji wa timu hiyo yenye makazi yake katika mitaa ya Msimbazi jijini Dar Es Salaam.