WINGA chipukizi wa kulia wa Azam FC, Arafat Ally Masoud 'Konde Boy' (18) amejiunga na klabu ya ENNPI ya Ligi Kuu Misri kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kudumu kwa miaka nane Chamazi.
Kwa mujibu wa vyanzo – Arafat aliyehitimu mafunzo ya kandansa katika akademi ya Azam FC mwaka 2024 – alisaini mkataba wa miaka mitatu Julai 26 kujiunga na Engineering for the Petroleum & Process Industries Sporting Club (ENPPI SC) ambao utafikia tamati Juni 30 mwaka 2028.