Msimamizi wa Clement Mzize, Jasmine Razack amefunguka MENGI kutoka moyoni lakini kubwa kwamba Yanga hawataki kumuuza mchezaji huyo na kilichobaki wanaleta usumbufu kwa kuongeza dau kubwa Ili timu zinazomtaka zishindww.
“Nimemchukua Clement Mzize wakati hana timu, Yanga walishamruhusu aondoke pale Under 20 ila Baba yake Mlezi pamoja na Kocha Zahera walikuja kuniomba sana nimchukue kumsimamia, hawajui namna gani Kijana ameteseka kufika alipo hapo, anategemewa na familia na yeye ndio kila kitu kwao, unadhani Yanga wamewekeza kiasi gani mpaka Mzize kufika hapo? Nafasi ya kuvunja Mkataba ipo ila kwasasa sitaki kumsumbua Kijana, acha alitumikie Taifa kwanza”
Jasmine Razack, Msimamizi wa Clement Mzize