RAIS Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace John Karia atagombea peke yake katika uchaguzi Mkuu wa shirikisho hilo Agosti 16, mwaka huu Jijini Tanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Kiomoni Kibamba ametoa orodha ya mwisho wa wagombea leo kufuatia wagombea walienguliwa kuwania nafasi hiyo, Dh. Mshindi Msolla na Shijja Richard kushindwa rufaa yao.
Wagombea wengine wote waliopitishwa ni wa nafasi za Ujumbe wa Kanda sita ambao wanaingia moja moja kwenye Kamati ya Kamati ya Utendaji.
Hao ni Lameck Nyambaya atakayechuana na CPA Hosseah Hopaje Lugani katika Kanda Namba 1 (Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtawra), Khalid Abdallah Mohamed anayegombea peke yake Kanda Namba 2 (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara), James Patrick Mhagama anayechuana na Evance Gerald Mgeusa na Cyprian Charles Kuyava Kanda Namba 3 (Ruvuma, Njombe, Mbeya, Songwe na Iringa).
Wengine ni Mohamed Omar Aden anayegombea peke yake Kanda Namba 4 (Dodoma, Singida, Shinyanga na Simiyu), Vedastus Kalwizira Lufano anayechuana na Salum Ally Kulunge Kanda Namba 5 (Mwanza Geita, Kagera na Mara) na Issa Mrisho Bukuku anayegombea peke yake Kanda Namba 6 (Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa).