Mohamed Hussein, alifunga bao lake la kwanza akiwa na timu ya taifa agosti 2,2025 katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya CHAN dhidi ya Burkinafaso.
Imemchukua zaidi ya michezo 40 ndani ya miaka takribani 10 kuifungia bao timu ya taifa ya Tanzania.
Mohamed ambaye mara nyingi amekuwa akitumika eneo la ulinzi wa kushoto alianza kuitumikia timu ya taifa rasmi novemba 22,2015 katika mchezo dhidi ya Somalia katika michuano ya CECAFA.
Huenda ukawa mwanzo mzuri kwa nyota huyu kuendelea kuifungia mabao muhimu timu ya taifa.