Msanii nyota wa Bongo Fleva, Rayvanny, amefichua kwa mara ya kwanza kuwa alilipa kiasi cha shilingi bilioni 1.3 za Kitanzania ili kuondoka rasmi kwenye lebo ya WCB Wasafi, licha ya hakukuwa na mkataba wowote wa kisheria wa rayvanny na lebo hiyo.
Rayvanny alijiunga na WCB mwaka 2015 na kupitia lebo hiyo, alifanikiwa kujizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania. Baada ya miaka kadhaa ya mafanikio, alianzisha lebo yake binafsi ya Next Level Music (NLM)