Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amewazadia Taifa Stars kiasi cha shilingi milioni 200 ikiwa ni motisha kuelekea mchezo wa robo fainali dhidi ya Morocco, utakaochezwa Ijumaa, Agosti 22, 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Fedha hizo zimewasilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, alipoitembelea timu hiyo kambini jijini Dar es Salaam, leo Agosti 20, 2025, na kuwapongeza kwa hatua kubwa waliyofikia pamoja na kuwatakia heri kwa mchezo ujao.